Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Oktoba 2, 2016
http://dollarcell.com/?ref=546220 TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI MUHTASARI WA MKATABA. 1. Bodi ya Wadhamini wa Young Africans Sports Club, (ambayo hapa inajulikana kama Mmiliki”) imeingia tarehe 3 September, 2016 Mkataba wa kukodishwa na kampuni ijulikanayo Yanga Yetu Limited (inayojulikana hapa kama “Mkodishwaji” kwa muhtasari wa maazimio yaliyoafikiwa katika Mkutano Mkuu wa Young Africans Sports Club uliofanyika tarehe 6 Agosti, 2016 ulitambua kuwa Young Africans Sports Club (anayejulikana hapa kama “YANGA”): 1.1 KWA KUWA, Timu ya Soka ya Mmiliki ni kongwe na yenye mafanikio kuliko timu ya soka nyingine zilizoko katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, yenye thamani kubwa kiutamaduni na kwa urithi wa Taifa, licha ya jitihada zake zote, inakabiliwa na changamoto za kifedha katika kuiendesha timu yake ya mpira wa miguu, kwa kuwa na usajili mdogo wa uanachama, ukosefu wa mapato, ya ada za Wanachama, mifumo isiyo na ufanisi ya kiuendeshaji, kushindwa kujipatia kipato cha kibiasha...